Pages

Powered by Blogger.

KAMA WEWE NI MJASIRIAMALI USIPITWE NA HII

Thursday, April 14, 2016

Tatizo la ajira ni wimbo unaoimbwa kila siku na watu wa rika na jinsia tofauti  huku watalaam wakishauri mtu mmoja mmoja kujiajiri kwa kufanya ujasiriamali mdogo na baadae kupiga hatua zaidi za kimaendeleo.

Kwa kuzingatia changamoto hiyo ya ajira Taasisi inayo jihusisha na wajasiriamali wadogo wadogo TAMFI kwa kushirikiana na Benki ya Citi, wameandaa  Tuzo za wajasiriamali  kwa mwaka 2016 ambapo wajasiriamali wabunifu watafaidika na tuzo hizo pamoja fedha kiasi cha Shilingi milioni 45 kwa ushindi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa TAMFI Winnie Terry amesema mashindano hayo yataanza Aprili hadi Juni  mwaka huu, ambapo fursa zitatolewa kuendana na idadi ya watu, kanda, jinsia na shughuli za kiuchumi, huku vigezo vya ushindi vikilenga biashara inayokua, faida, ubunifu, na fursa za ajira zitakazopatikana kupitia biashara ya mjasiriamali.

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa mpango wa tuzo hizo za wajasiriamali utahakikisha unahusisha na kuwatambua wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa kuzingatia nguvu zao katika kuibua biashara miongoni mwa jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Citi Benki, Frank Kallage amesema benki yao itaendelea kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo kwani wamewekeza fedha zakutosha takriban milioni 100 za Kitanzania ili kujumuisha wadau muhimu ambao watashawishi muiondombinu sera na kanuni zinazoruhusu ubunifu duniani kote.

No comments:

Post a Comment

 

Tafuta Blog Hii

Find us on Facebook

Tangaza Nasi Hapa

Umeisha Soma Hizi