Pages

Powered by Blogger.

JINSI YA KUMVUTIA MWANAMKE AMBAYE TAYARI ANA MPENZI

Wednesday, August 31, 2016

Image result


1. Kuwa mwanaume ambaye anakuwa kwa ndoto ya kila mwanamke uwa na tabia za kiume.

Kuwa ‘gentleman’ itamfanya mwanamke yeyote yule akuwaze na kukutia ndotoni mwake na pia kutaka kukujua zaidi kuwa mnakutana mara kwa mara.

Hakikisha ya kuwa unapenda kuwa karibu na yeye na akianza kuonyesha dalili zozote zile, mfano kukupa busu kwenye paji au shavuni, au kupenda kukukumbatia, fahamu kuwa unaenda sambamba na ajenda yako, Pia kumfanya akuweke kwa akili yake lazima uonyeshe hisia zako kwake.

2. Usiache kumuangalia
Wakati ambapo mnakuwa pamoja mnaongea, hakikisha kuwa macho yako yote yanamuangalia yeye kila wakati, Hii ni ishara ambayo itamuonyesha yeye kuwa una macho ambayo yanamzimia yeye peke yake, mbinu hii itamfanya kwa urahisi kutaka kutia machoni akuangalie kama bado tabia ya kumuangalia yeye uko nayo au la.

3. Usisahau kutumia lugha za kumsifu
Ukweli usemwe, watu wakiwa katika mahusiano kwa muda mrefu kuna vitu ambavyo wanavichukulia kama mzaha, Mfano katika mahusiano ya mwanamke na mwanamume, unakuta mara nyingi wamezoeana kiasi cha kuwa wanajihisi uhusiano wao umeshikana kiasi cha kuwa wanasahau mambo madogo madogo kama vile kumsifu mpenzi wake.

Hii ni njia wapo rahisi ambayo itakuwezesha wewe kuuteka moyo wa mwanamke ambaye ana mpenzi kwa haraka, Maneno ya kumsifu ambayo hajaambiwa kitambo yanaweza kumchanganya akili mwanamke yeyote na kumfanya kuingiwa na hisia mbili mbili. Niamini ukitumia mbinu hii utakuwa na nafasi kubwa ya kwako kufaulu kumpata mwanamke wa aina hii.

4. Hakikisha umemuelewa ndani na nje
Wengi wangeuliza itakuwaje kumfahamu mwanamke ndani na nje na tayari ana mpenzi? Kama ulikuwa hujui basi ni hivi, kulingana na utafiti, inasemekana kuwa akili ya mwanamke inafanya kazi tofauti kabisa na ya mwanamume, Kwahiyo usitilie shaka kabisa hapa, Pia hakikisha umesikiliza kila kitu ambacho atakwambia na utilie maanani yote atakayosema.

No comments:

Post a Comment

 

Tafuta Blog Hii

Find us on Facebook

Tangaza Nasi Hapa

Umeisha Soma Hizi