Takwimu za nchi nzima zinaonesha kwa mwaka 2013 zilitokea ajali 23,842 zilizosababisha vifo 4,002 na majeruhi 20,689. Mwaka 2014 zilitokea ajali 14,360 zilizosababisha vifo 3,760 na majeruhi 14,530 na mwaka 2015 zilitokea ajali 8,337 zilizosababisha vifo 3,468 na majeruhi 9,383,” hiyo ni kauli yake Hamad Yusuf Masauni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alipokuwa akizungumza bungeni mjini Dodoma.
Inauma na kusikitisha sana kuona idadi kubwa ya vifo ambavyo mara nyingi vimeripotiwa ni uzembe wa madereva ambao hujisahau kwamba wamebeba roho za watu kiasi cha kuamua kukatili maisha ya watu wasio na hatia.
Kwa mfano tukio la kusikitisha la hivi karibuni la mabasi mawili yanayomilikiwa na Kampuni ya City Boy yaliyogongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya wananaume 21 na wanawake 9 huko Maweni Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida chanzo kikitajwa kuwa mwendokasi na uzembe wa madereva kwa kufanya mzaha pindi wawapo barabarani. Hivi inawezekanaje wafikie hatua ya kufanya majaribio na maisha ya watu?
Ili kudhibiti matukio haya na kuwatia nguvuni wale wote wanaofanya mzaha mzaha na mwisho wa siku usaha kuwatumbukia hizi hapa namba za simu za Makamanda wa Polisi Mikoa ambazo ukipiga kuripoti pale unapoona mambo yanakwenda ndivyo sivyo utafanikiwa kuokoa maisha yako na ya wengine.
CHARLES MKUMBO – RPC ARUSHA 0715 009 912
AHMED MSANGI – RPC MWANZA 0715 009 949
FERDINAND MTUI – RPC KIGOMA 0715 009 915
GEORGE KYANDO – RPC RUKWA 0715 009 954
AUGUSTINO OLLOMI – RPC KAGERA 0715 009 916
No comments:
Post a Comment