Umekutana na msichana wa sampuli uliyokuwa ukiiota tangu utoto wako na ame kukubalia kuwa atakuwa mpenzi wako, au pengine tayari mmekubaliana kufunga ndoa, Hiyo ni hatua kubwa ambayo unapaswa kujipongeza kwa kuifikia, kwani si wote wanaoweza kufanikiwa kuwapata wanawake walio katika viwango walivyovitaka wao. Hata hivyo, unakabiliwa na mtihani mwingine.
Ni msichana unayempenda sana na umepanga kuwa umpe mapenzi ya hali ya juu, katika maisha ya kawaida na kitandani pia. Pengine katika mazungumzo yako pia uliashiria kuwa ni mjuzi katika suala zima la mapenzi.
Vilevile, yamkini akilini mwako umejijengea mawazo kuwa njia ya kwanza kabisa ya kumwonesha msichana wako kuwa kwako amefika, ni kumpagawisha kimapenzi unapokutana naye kimwili kwa mara ya kwanza.
Ni ukweli usiopingika kuwa mapenzi ya siku ya kwanza ni ya kihistoria hasa kwa mwanamke na kuna makubaliano miongoni mwa wataalamu wa saikolojia ya mapenzi kuwa mwanamke anapo furahishwa siku ya kwanza hujenga mapenzi makubwa kwa mwanaume aliyempa furaha hiyo, hususani kama ni mara yake ya kwanza kufanya mapenzi.
Sasa je, uko tayari kuona mwanamke uliyemhangaikia kwa siku nyingi mpaka akakukubalia anakata tamaa na kukupuuza siku ya kwanza tu ya kukutana nawe? Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayetamani kuingia katika hali hii.
Ni wazi kuwa ungependa kujijengea jina na mapenzi makubwa kwa mwanamke wako huyu maridadi. Ili kukusaidia wewe ambaye umempata mpenzi na una wasiwasi kuwa pengine unaweza kuvuruga kila kitu katika siku ya kwanza, hapa yatabainishwa mambo mawili ambayo ukiyazingatia hutapaswa kuwa na shaka.
Lakini hatua ya kwanza kabisa ni kujisikia huru. Suala la kukutana kwa mara ya kwanza na mpenzi huonekana kuwatisha wengi kuliko inavyopaswa. Katika kukabiliana nalo, jisikie huru kwanza na nafsi yako, kisha na mtu uliye naye, halafu mambo mengine yatafuata.
Usihofie maumbile yako, Baadhi ya wanaume huwa na wasiwasi na maumbile yao. Katika zama hizi habari kuhusiana na masuala ya maumbile zimetapakaa kila mahala na mtu anaweza kujilinganisha na kujiona kama yeye hafai, mathalani ni mfupi. Kwa sababu hiyo, mwanaume atakuwa na wasiwasi kuwa mpenzi wake ‘hatamtambua’ vizuri, hususani katika siku hiyo ya kwanza na pengine huo utakuwa mwanzo wa kumdharau kisha kumwacha.
No comments:
Post a Comment