Pages

Powered by Blogger.

YAKUZINGATIA UNAPOKUTANA KIMWILI NA MWANAMKE SIKU YA KWANZA

Thursday, September 1, 2016

Image result

Umekutana na msichana wa sampuli uliyokuwa ukiiota tangu utoto wako na ame kukubalia kuwa atakuwa mpenzi wako, au pengine tayari mmekubaliana kufunga ndoa, Hiyo ni hatua kubwa ambayo unapaswa kujipongeza kwa kuifikia, kwani si wote wanaoweza kufanikiwa kuwapata wanawake walio katika viwango walivyovitaka wao. Hata hivyo, unakabiliwa na mtihani mwingine.

Ni msichana unayempenda sana na umepanga kuwa umpe mapenzi ya hali ya juu, katika maisha ya kawaida na kitandani pia. Pengine katika mazungumzo yako pia uliashiria kuwa ni mjuzi katika suala zima la mapenzi.

Vilevile, yamkini akilini mwako umejijengea mawazo kuwa njia ya kwanza kabisa ya kumwonesha msichana wako kuwa kwako amefika, ni kumpagawisha kimapenzi unapokutana naye kimwili kwa mara ya kwanza.

Ni ukweli usiopingika kuwa mapenzi ya siku ya kwanza ni ya kihistoria hasa kwa mwanamke na kuna makubaliano miongoni mwa wataalamu wa saikolojia ya mapenzi kuwa mwanamke anapo furahishwa siku ya kwanza hujenga mapenzi makubwa kwa mwanaume aliyempa furaha hiyo, hususani kama ni mara yake ya kwanza kufanya mapenzi.

Sasa je, uko tayari kuona mwanamke uliyemhangaikia kwa siku nyingi mpaka akakukubalia anakata tamaa na kukupuuza siku ya kwanza tu ya kukutana nawe? Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayetamani kuingia katika hali hii.

Ni wazi kuwa ungependa kujijengea jina na mapenzi makubwa kwa mwanamke wako huyu maridadi. Ili kukusaidia wewe ambaye umempata mpenzi na una wasiwasi kuwa pengine unaweza kuvuruga kila kitu katika siku ya kwanza, hapa yatabainishwa mambo mawili ambayo ukiyazingatia hutapaswa kuwa na shaka.

Lakini hatua ya kwanza kabisa ni kujisikia huru. Suala la kukutana kwa mara ya kwanza na mpenzi huonekana kuwatisha wengi kuliko inavyopaswa. Katika kukabiliana nalo, jisikie huru kwanza na nafsi yako, kisha na mtu uliye naye, halafu mambo mengine yatafuata.

Usihofie maumbile yako, Baadhi ya wanaume huwa na wasiwasi na maumbile yao. Katika zama hizi habari kuhusiana na masuala ya maumbile zimetapakaa kila mahala na mtu anaweza kujilinganisha na kujiona kama yeye hafai, mathalani ni mfupi. Kwa sababu hiyo, mwanaume atakuwa na wasiwasi kuwa mpenzi wake ‘hatamtambua’ vizuri, hususani katika siku hiyo ya kwanza na pengine huo utakuwa mwanzo wa kumdharau kisha kumwacha.


JINSI YA KUMVUTIA MWANAMKE AMBAYE TAYARI ANA MPENZI

Wednesday, August 31, 2016

Image result


1. Kuwa mwanaume ambaye anakuwa kwa ndoto ya kila mwanamke uwa na tabia za kiume.

Kuwa ‘gentleman’ itamfanya mwanamke yeyote yule akuwaze na kukutia ndotoni mwake na pia kutaka kukujua zaidi kuwa mnakutana mara kwa mara.

Hakikisha ya kuwa unapenda kuwa karibu na yeye na akianza kuonyesha dalili zozote zile, mfano kukupa busu kwenye paji au shavuni, au kupenda kukukumbatia, fahamu kuwa unaenda sambamba na ajenda yako, Pia kumfanya akuweke kwa akili yake lazima uonyeshe hisia zako kwake.

2. Usiache kumuangalia
Wakati ambapo mnakuwa pamoja mnaongea, hakikisha kuwa macho yako yote yanamuangalia yeye kila wakati, Hii ni ishara ambayo itamuonyesha yeye kuwa una macho ambayo yanamzimia yeye peke yake, mbinu hii itamfanya kwa urahisi kutaka kutia machoni akuangalie kama bado tabia ya kumuangalia yeye uko nayo au la.

3. Usisahau kutumia lugha za kumsifu
Ukweli usemwe, watu wakiwa katika mahusiano kwa muda mrefu kuna vitu ambavyo wanavichukulia kama mzaha, Mfano katika mahusiano ya mwanamke na mwanamume, unakuta mara nyingi wamezoeana kiasi cha kuwa wanajihisi uhusiano wao umeshikana kiasi cha kuwa wanasahau mambo madogo madogo kama vile kumsifu mpenzi wake.

Hii ni njia wapo rahisi ambayo itakuwezesha wewe kuuteka moyo wa mwanamke ambaye ana mpenzi kwa haraka, Maneno ya kumsifu ambayo hajaambiwa kitambo yanaweza kumchanganya akili mwanamke yeyote na kumfanya kuingiwa na hisia mbili mbili. Niamini ukitumia mbinu hii utakuwa na nafasi kubwa ya kwako kufaulu kumpata mwanamke wa aina hii.

4. Hakikisha umemuelewa ndani na nje
Wengi wangeuliza itakuwaje kumfahamu mwanamke ndani na nje na tayari ana mpenzi? Kama ulikuwa hujui basi ni hivi, kulingana na utafiti, inasemekana kuwa akili ya mwanamke inafanya kazi tofauti kabisa na ya mwanamume, Kwahiyo usitilie shaka kabisa hapa, Pia hakikisha umesikiliza kila kitu ambacho atakwambia na utilie maanani yote atakayosema.

LYRICS: Diamond Platnumz – Kidogo Ft. P-Square

Friday, July 15, 2016

Lyrics Of Kidogo By Diamond Platnumz Ft. P-Square

[Intro]
Eeeh
P-Square and Diamond
Wasafi
[Pre-Chorus]
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo
[Hook – Diamond Platnumz & P-Square]
She gat me
Dancing eeh
Party eeh
Fiesta eeh
Forever aah
Ooh yeaaaaah
Yani kabisa mi ananimalizaga
Dancing eeh
Party eeh
Fiesta eeh
Forever aah
Ooh yeaaaaah
Yani kabisa mi ananimalizaga
[Chorus]
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (basi nipe kidogo mama)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (nipe tenaa)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (basi nipe kidogo mama)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo
[Verse 1 – P-Square & Diamond Platnumz]
Oya come make we gum body (ooh yeah)
You and I we become body (ooh yeah)
Girl as you dey see me so (ooh yeah)
I Will never let you go tai (ooh yeah)
Mpaka napata midadii (ooh yeah)
Wapi unataka mikadii (ooh yeah)
Aah kote mi nipo (ooh yeah)
Say my beautiful (ooh yeah)
I’m in love (I’m in loooove)
I’m gonna give you what your need
Lemme give you what you need
I’m in love (I’m in loooove)
I’m gonna give you what your need
Lemme give you what you need
[Hook – Diamond Platnumz & P-Square]
She gat me
Dancing eeh
Party eeh
Fiesta eeh
Forever aah
Ooh yeaaaaah
Yani kabisa mi ananimalizaga
Dancing eeh
Party eeh
Fiesta eeh
Forever aah
Ooh yeaaaaah
Yani kabisa mi ananimalizaga
[Chorus]
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (basi nipe kidogo mama)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (nipe tenaa)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (basi nipe kidogo mama)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo
[Verse 2 – Diamond Platnumz & P-Square]
Wasije kwa ngongongo kerewa haa
Minjonjo ukalewa hee
Mwishoni ukanogewa hehehe
Na tunda nikamegewa eeeh
Chululi si ndondondo chelewa haa
Ni uwongo elewa hee
Chonde chonde mamy hehehe
Utanikoseaa
Oya come make we gum body (ooh yeah)
You and I we become body (ooh yeah)
Girl as you dey see me so (ooh yeah)
I Will never let you go tai (ooh yeah)
Mpaka napata midadii (ooh yeah)
Wapi unataka mikadii (ooh yeah)
Aah kote mi nipo (ooh yeah)
Say my beautiful (ooh yeah)
I’m in love (I’m in loooove)
I’m gonna give you what your need
Lemme give you what you need
I’m in love (I’m in loooove)
I’m gonna give you what your need
Lemme give you what you need
[Hook – Diamond Platnumz & P-Square]
She gat me
Dancing eeh
Party eeh
Fiesta eeh
Forever aah
Ooh yeaaaaah
Yani kabisa mi ananimalizaga
Dancing eeh
Party eeh
Fiesta eeh
Forever aah
Ooh yeaaaaah
Yani kabisa mi ananimalizaga
[Chorus]
Kidogo dogo (eeeeh)
Kidogo dogo (eeeeh)
Kidogo dogo (kidogo dogo mamaaa)
Kidogo dogo (unanichangaya kabisaa)
Kidogo dogo (usiki kucha na na kukicha)
Kidogo dogo (eeeeh)
Kidogo dogo (aah kirangaraa)
Kidogo dogo
[Verse 3 – P-Square & Diamond Platnumz]
Tonight, i’m gonna give you all the love you deserve
Nobody can take it awaaaay
My baby you look so fine (so fine)
My african girl so beautiful (so beautiful)
I’m in love, You’re in love
So in love, yeaah
I’m in love, You’re in love
So in love
Yani kabisa ananimalizaga
[Chorus]
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (aah kidogo kile)
Kidogo dogo (aah kidogo mama)
Kidogo dogo (ooh yeah)
Kidogo dogo (ooh yeah)
Kidogo dogo (ooh yeah)
Kidogo dogo (ooh yeah)
Kidogo dogo (ooh yeah)
Kidogo dogo (ooh yeah)
Kidogo dogo (ooh yeah)
Kidogo dogo (ooh yeah)
[Outro]
WASAFI!!!

Mtv Base walivyoisifia video mpya ya Diamond ‘Kidogo’ na kumuita mfalme wa…..

Thursday, July 14, 2016



Kituo cha tv cha kimataifa MTV Base kimeipa sifa kubwa video mpya ya Diamond Platnumz aliyowashirikisha P Sqaure kutoka Nigeria. Video hii ni KIDOGO.
Ukiacha kuipa sifa kuwa ndio video bora kwa sasa AFRICA ila pia MTV Base wanasema Diamond ndio MFALME WA MUZIKI WA AFRICA MASHARIKI‘King OF East African Music’

ILI KUNUSURU MAISHA YAKO NA YA WENGINE, SOMA HII

Friday, July 8, 2016

Takwimu za nchi nzima zinaonesha kwa mwaka 2013 zilitokea ajali 23,842 zilizosababisha vifo 4,002 na majeruhi  20,689. Mwaka 2014 zilitokea ajali 14,360 zilizosababisha vifo 3,760 na majeruhi 14,530 na mwaka 2015 zilitokea ajali 8,337 zilizosababisha vifo 3,468 na majeruhi 9,383, hiyo ni kauli yake Hamad Yusuf Masauni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alipokuwa akizungumza bungeni mjini Dodoma.


Inauma na kusikitisha sana kuona idadi kubwa ya vifo ambavyo mara nyingi vimeripotiwa ni uzembe wa madereva ambao hujisahau kwamba wamebeba roho za watu kiasi cha kuamua kukatili maisha ya watu wasio na hatia.

Kwa mfano tukio la kusikitisha la hivi karibuni la mabasi mawili yanayomilikiwa na Kampuni ya City Boy yaliyogongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya wananaume 21 na wanawake 9 huko Maweni Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida chanzo kikitajwa kuwa mwendokasi na uzembe wa madereva kwa kufanya mzaha pindi wawapo barabarani. Hivi inawezekanaje wafikie hatua ya kufanya majaribio na maisha ya watu?

Ili kudhibiti matukio haya na kuwatia nguvuni wale wote wanaofanya mzaha mzaha na mwisho wa siku usaha kuwatumbukia hizi hapa namba za simu za Makamanda wa Polisi Mikoa ambazo ukipiga kuripoti pale unapoona mambo yanakwenda ndivyo sivyo utafanikiwa kuokoa maisha yako na ya wengine.

CHARLES MKUMBO – RPC ARUSHA 0715 009 912

AHMED MSANGI – RPC MWANZA   0715 009 949

FERDINAND MTUI – RPC KIGOMA  0715 009 915

GEORGE KYANDO – RPC RUKWA   0715 009 954

AUGUSTINO OLLOMI – RPC KAGERA  0715 009 916

Vanesa ajibu mapigo kwa shilole

Wednesday, May 18, 2016


Zinachukuliwa na Warembo kudoka Kiwanda cha Bongoflevani na hii ni baada ya May 17 2016 Shilole kupost picha kwenye Account yake Instagram ambayo wengi wametafsiri ni dongo kwa msanii mwenzake Vanessa Mdee, May 18 2016 Vanessa Mdee amezichukua headline kwa Kupost picha ya Shilole na kuandika caption inayosomeka hivi.
‘Nikupe KICKII ujulikane au sio? Kila siku twanyamazaga ndiyo mtugaragaze. Sit the f**k down. Mimi sio uliowazoea. P.s: You ain’t worth this post inashushwa sasa hivi #MessageSent‘>>>Vanessa Mde

UNACHOTAKIWA KUFANYA PALE UNAPOANZISHA BIASHARA

Thursday, April 14, 2016

Najua nazungumza na mabilionea wakubwa, kama si mabilionea wa sasa, basi ni mabilionea wa baadaye. Wewe ni bilionea, nakutamkia hili na unatakiwa kuamini pasipo kujali kwamba kwenye akaunti una shilingi elfu moja au chini ya hapo, unachotakiwa kuamini kwamba wewe ni bilionea.
Inawezekana umeanzisha biashara yako, kitu cha ajabu kabisa, fedha hazikai, kila ukipata leo, kesho hazipo, ili kuendesha biashara yako inakupasa kukopa sehemu, ni kweli ulipata faida, ila kwa nini ukope? Kopa wakati ukitafuta mtaji, ila kama umeshafanya biashara na faida ukapata, kwa nini ukope? Kwa nini usitumie faida uliyoipata kukuinua hapo ulipo?
Wengi wanakutana na hali hiyo, si wewe tu, hata mimi nilishawahi kukutana nayo, na si sisi tu, amini hata mabilionea wakubwa walishawahi kukutana na hali hiyo. Hivi unajua ni mabilionea wangapi waliwahi kufilisika? Unamjua Muitaliano Enzo Ferrari? Alipata fedha, akafilisika, akagundua alipofanya makosa, akatafuta tena, akazipata.
Wewe kama binadamu wengine, unaweza kupata fedha na kufilisika, hapa siwazungumzii wakina Bakhresa, Mengi na wengineo, nakuzungumzia wewe mwenye biashara ndogo, nataka biashara yako ikue, utoke hapo ulipo na usogee mbele zaidi, ufanikiwe na siku moja uitwe bilionea Omari, Selemani, John, Hamisi, Sara, Anna, Peter au jina lolote ulilokuwa nalo.
Hizi ni baadhi ya njia ambazo zinaweza kukusaidia kufikia ubilionea japokuwa una biashara ndogo au kipato kidogo.
1. WEKA MALENGO: Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya kama mfanyabiashara ni kuweka malengo. Hebu chukua karatasi, andika malengo yako na kuyafanyia kazi. Kumbuka wewe ni bilionea, usiweke malengo ambayo unadhani kwamba pia ua utayafikia, ukiyaandika hayo, jua hautotoa nguvu kubwa kupambana ili uyafikie malengo hayo. Kama una mtaji mdogo, weka malengo makubwa ya kufanikiwa, unapoweka malengo makubwa zaidi ya ulichonacho kitakufanya ujitoe zaidi, uongeze juhudi ili kufikia kile unachokiwazia.
Mfano wewe ni mfanyabiashara mdogo, ukaweka lengo kwamba mpaka mwaka kesho lazima uanzishe biashara ya kuuza mahindi mitaani. Sawa, si vibaya lakini ulitakiwa kuweka malengo ya biashara kubwa zaidi. Kwa fedha hizohizo ulizokuwa nazo, unaweza kuanzisha biashara ya mahindi, ukijiwekea hivyo, jua kwamba unayachelewesha mafanikio yako. Ninataka ujitume kwa nguvu zote, ukiweka yale malengo makubwa, utajiona huwezi kufika lakini ndiyo yatakayokufanya kupambana zaidi, hutolala, utapambana usiku na mchana ila ukiweka lengo dogo, utasema subiri upumzike kwani lengo hilo litakuja hata kama hutojitoa, hivyo ili ufanikiwe, jiwekee lengo kubwa na hakika utapiga hatua.
Mfano mzuri mimi. Sikuwa na fedha kipindi cha nyuma, ishu ya kuanzisha magazeti ilihitaji msingi mkubwa sana, ila sikutaka kukwepa lengo langu la kufanya hivyo. Ningeweza kusema niuze machungwa mitaani, kweli ningeuza, lakini kwa nini niweke lengo dogo? Je ningejitoa zaidi? Ili nijitoe, ili nifanye kazi usiku na mchana ilikuwa ni lazima niweke lengo kubwa, nikaweka, nikajitoa na kufanikiwa. Kama Shigongo, yule mtoto masikini ameweza, vipi kuhusu wewe?
2. USIOGOPE KUFELI: Ndiyo! Kuna watu waoga sana, wanaogopa kufanya biashara fulani kubwa kwa kuwa wanaogopa kuanguka. Rafiki yangu, kuanguka ni sehemu moja ya maisha, ili usonge mbele ni lazima uanguke. Huwezi kujua kuendesha baiskeli kama hujaanguka, ni lazima uanguke ili ujue, iko hivyo.
Mtoto anapoanza kutembea, kuna kipindi anaanguka, mbona yeye hakati tamaa na kusema kwamba kuanzia leo hatembei tena kisa ameanguka? Akianguka, hunyanyuka na kutembea tena, akianguka anajaribu tena.
Wewe kama mfanyabiashara mdogo au mkubwa, jifanye mtoto, usiogope kufeli, ili usonge mbele, ni lazima ufeli, huwezi kuwa mshindi siku zote, kuna kipindi unashindwa, ukishindwa, unakaa chini na kuwaza umeshindwa wapi, unajipanga na kurudi tena kwenye gemu.
Kama ningekuwa naogopa kufeli, nakwambia ukweli kwamba nisingekuwa hapa, labda leo ningekuwa mtaani tu nafanya biashara ndogondogo, kuogopa kufeli kungenifanya niwe kulekule nilipokuwa nyuma. Ili ujifunze, ili upige hatua ni lazima ufeli, ukifeli, unajifunza na kusonga mbele.
3. WEKA UMAKINI NA FEDHA ZAKO: Siku zote nimekuwa nikiwaambia watu, si vizuri kutumia kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya unachoingiza. Mwingine ana biashara inaingiza elfu ishirini kwa siku, ila anataka kufanya matumizi yasiyokuwa na faida kwa kutumia elfu thelathini. Ndugu yangu! Huwezi kuishi kwa maisha haya halafu ukaja kufanikiwa. Unatakiwa kuwa makini na fedha zako.
Mwingine anasema, nimepata faida nyingi, acha nikale bata! Ndugu zangu, bata haziishi, kila siku zinaongezeka, baa hazifungwi, umezikuta na utaziacha, kumbi za starehe kila siku zinafunguliwa mpya.
Ithamini pesa yako, hata kama ni shilingi hamsini, ithamini. Unapokuwa na elfu moja, inayokamilisha hela hiyo ni shilingi hamsini, kama ukiwa na 950, huwezi kupata 1000 kama huna hamsini, kwa hiyo kwenye maisha yako ya kibiashara, hata shilingi 50 ni muhimu mno kwako.
Usiipuuzie fedha yoyote ile, panga matumizi yako ya kawaida, si muhimu sana kunywa soda kama huna sababu ya kufanya hivyo! Hakuna umuhimu wa kula chipsi kuku kama hakuna umuhimu wa kufanya hivyo! Kwani usipokula chipsi kuku utakufa? Kama una kiasi kidogo cha fedha basi hata matumizi ya fedha yako hakikisha yanakuwa madogo na si makubwa zaidi ya kile ulichokipata.
4. JENGA URAFIKI NA WENYE FEDHA: Hapa simaanishi kwamba wasiokuwa na fedha inabidi watengwe, hapana! Ila unatakiwa kuwa makini, ni vizuri kutengeneza marafiki wapya lakini inabidi uwe makini. Kabla ya kuwa nilivyo niliwahi kuwasikia watu wakisema unapoanza kufanikiwa unabadilika, nilipinga lakini nikaja kuona inawezekana.
Unapokuwa umefika hatua fulani, automatic unaanza kutafuta watu ambao wanaweza kukuvusha kutoka hapo ulipo, watu wenye uwezo wa kukufanya kufanikiwa zaidi. Kumbuka shuleni kwenu, ni wanafunzi wangapi waliokuwa na akili walikuwa marafiki wao kwa wao? Kwani hawakuwa marafiki zako pia, walikuwa marafiki zako ila wenyewe wakawa beneti, ipo hivyo.
Unapopata fedha, unapofanikiwa, jaribu kutengeneza ukaribu na watu waliofanikiwa, usiwaache wale wengine, kuwa nao ila usiwe nao beneti kupindukia, kama unaona mtu haeleweki, hana hamasa ya kukufanya kufanikiwa, kwa nini uwe naye beneti? Muache awe rafiki wa kupiga naye stori dakika kumi na kuondoka.
Unapokuwa siriazi kutafuta fedha, huna budi kuwatafuta waliofanikiwa, wakufundishe kwa nini wapo hapo, walipitia nyanja zipi mpaka kufanikiwa hivyo? Ni lazima ujifunze kupitia wao na hakika utafanikiwa.
5. USICHANGANYE BIASHARA NA URAFIKI/NDUGU: Ndiyo! Wengi tunafeli hapa. Tunapopata nafasi ya kufanya biashara, wengi tunakosa kufanikiwa kwa sababu tu tumechanganya urafiki katika biashara. Biashara ndogo lakini bado unataka kukopesha, tena kwa watu ambao huna uhakika kama watakulipa.
Unapoanzisha biashara, wengi watakuja kukopa na si kununua, hebu jiulize, wakati hujaanzisha hiyo biashara, mbona hawakuwa wakienda kukopa sehemu nyingine? Jua sisi binadamu tuna makusudi, tunapomuona mtu ameanzisha biashara, mara nyingi tunataka kumuangusha chini ili tumcheke, tumdhihaki kwamba kiko wapi sasa! Unatakiwa kuwa makini sana, huu si muda wa kupeleka urafiki na undugu katika biashara. Unapoanzisha biashara na ikatokea umemuajiri ndugu yako, mwambie wazi kwamba upo kama mfanyabiashara na si kama ndugu, anapofanya makosa, mchukulie hatua kama unavyomchukulia mtu baki, ukimuacha kwa kuogopa lawama, huyohuyo baadaye atakuja kukucheka.
Unapoona una hamu ya kula chipsi, na wewe unaifanya biashara hiyo ya chipsi, nunua chipsi zako, si kwamba ni zako basi na wewe ule bure. Najua ni ngumu kwa watu wengine lakini inabidi ufanye hivyo ili kuifanya biashara yako isimame.
Leo unapouza chipsi na kula bure, amini kwamba kesho utataka uongeze na chipsi yai, keshokutwa chipsi samaki, sasa ukifanya hivyo, hutofanikiwa kwa hiyo ni lazima hata wewe mwenyewe ujidai.
Sina mengi, ila tukutane muda mwingine kwa makala nyingine ya ujasiriamali. Kumbuka, wewe ni bilionea, fanya mambo kama bilionea.
Page 1 of 5123...5
 

Tafuta Blog Hii

Find us on Facebook

Tangaza Nasi Hapa

Umeisha Soma Hizi